KITENGO CHA SHERIA
Kitengo cha sheria cha Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni kati ya vitengo vyenye hadhi sawa na idara vilivyoundwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kikiwa na majukumu mbalimbali. Kitengo cha sheria kimeundwa na mkuu wa kitengo akisaidiwa na wanasheria wawili.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA:-
1.Kutoa ushauri kwa masuala yote ya kisheria kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na kwa wakuu wote wa idara (HODs)wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
2.Kuiwakilisha Halmashauri Mahakamani katika mashauri yote yanayoihusu Halmashauri kwa maana ya kushtaki au kushtakiwa.
3.Kufanya Mapitio ya Uhalali wa mikataba kwa mujibu wa sheria na kuandaa mikataba mbalimbali inayoihusu Halmashauri au Taasisi zake.
4.Kuandaa sheria ndogo za halmashauri na sheria ndogo za Vijiji vilivyoko ndani ya eneo la Halmashauri.
5.Kusimamia na kutoa mafunzo ya uendeshaji wa mabaraza ya kata wilayani Shinyanga.
6. Kuratibu na kusajili vyombo vya watumia maji wilayani Shinyanga.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.