• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Shinyanga District Council
Shinyanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Nice, awataka Madiwani kubuni Vyanzo vipya vya Mapato na kusimamia vIzuri vyanzo Vilivyopo

Posted on: August 20th, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ndg Nice R. Munissy, Aliongoza vyema Baraza lake la Kwanza kama Katibu wa Baraza la Madiwani. Akisoma Salamu zake kwa Baraza hilo mara tu baaada ya Sala ya kuiombea Halmashauri iliyosomwa na Mstahiki Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa S. Mboje, Ndugu Nice wakati akiwasilisha salaam, Alianza kwa Kumshukuru sana Mhe. Rais SAMIA SULUHU HASSAN  kwa Kumteuwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kisha Aliwaomba Madiwani wampe Ushirikiano kwenye kutekeleza Majukumu yake kama Mkurugenzi.

"Tumekuja Kusimamia Shughuli za Halmashauri na Serikali kwa ujumla, ni matumaini yangu tutabainisha Shughuli zote muhimu na kuanza kuzisimamia lakini Nasisitiza Mkazo uwe ni kwenye kukusanya Mapato na kuhakikisha Fedha ya Serikali tunayoikusanya inatumiwa vizuri" Alisisitiza Mkurugenzi huyo Kijana.

Mkurugenzi huyo pia aliwaomba sana Waheshimiwa Madiwani kuwa wakali kwenye Maeneo yao na kutowa usimamizi unaohitajika kuhakikisha Miradi ya Serikali inakamilishwa kwa wakati, viwango na ubora unaohitajika. "Serikali inatowa pesa nyingi kwa Ajili ya Miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yenu, nawakumbusha na ni wajibu wenu kuhakikisha mnakuwa Wakali kwenye hii miradi ili ilete tija inayohitjika. nitasikitika sana kusikia Mradi haukwenda vizuri kwenye Eneo la Mhe. Diwani wakati yeye na Team yake ya Kata wapo na walikuwa wakiangalia tu" Aliwataka Waheshimiwa Madiwani kuwa wakali kwenye usimamizi wa Miradi ya Serikali.

Akisitiza tena kwenye Ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya Mapato. Mkurugunzi huyo mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga alisema" Nawaomba Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wetu, kuwa wabunifu sana kwenye kuunda vyanzo vipya vya Mapato kwenye maeneo yetu, nakuhakisha tunasimamia ipasavyo vyanzo vilivyopo. " Ofisi yangu itatowa ushirikino wa Hali na Mali kuhakikisha tunalinda vyanzo vyetu vya Mapato vilivopo na kubuni vyanzo vipya vya Mapato  katika Halmashauri yetu. Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassani ametuamini na nawahakikishia hatutamuangusha kwenye usimamizi wa Makusanyo ya Serikali na kuhakikisha tunatumia vyema mapato tunayoyakusanya.

kwa upande wao waheshimiwa Madiwani walieleza kero za Wananchi kwenye Baraza hilo na kuitaka Serikali ipatie Ufumbuzi haraka migogoro hiyo. wakiitaja baadh ya Migogoro waheshimiwa Madiwani walisema kuna mgogoro wa mipaka kati ya Wananchi wa Kata za Nyamalogo, Mwalukwa, Pandagichiza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ). "mgogoro huu umeanza kutishia usalama wa Raia na Mali zao. kuna baadhi ya wananchi wanakata miti yao na kutenegeneza kuni, lakini wanajeshi wanawanyang'anya kuni hizo wakidai maeneo hayo ni ya jeshi." Alisema Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Mwalukwa.

Lakini pia walieleza kero kubwa kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuwa ni Suala la uuzaji wa mazao ghalani. mheshimiwa DAS, Mheshimiwa Muwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, na Ndg. Mkurugenzi, "tunaomba hili swala la bei ya mazao hasa ya Choroko na Dengu lipatiwe ufumbuzi haraka. wananchi wakiuza kwa wafanya biashara bei inakuwa nzuri mpaka Sh. 1600 wakati mwengine lakini wakiuza kwa hawa sijui mnawaita AMCOS ambao ndio wanunuzi walioidhinishwa basi bei inashuka mpaka kufikia Sh. 800. hivi hizi ni hesabu gani?" Alisisitiza Mhe. Sengerema, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Iselamagazi.

Akijibu kero hizo, Mheshimiwa DAS wa Wilaya ya Shinyanga alisema Serikali imeanza kuzitafutia Ufumbuzi na kuahidi kuwa Kwenye Baraza lijalo watakuja na Majawabu yaliyofanyiwa tathimini ya uhakika na utatuzi wa kero hizo. "Tutashirikiana na Wataalam wetu, wahusika wote wa Mgogoro hiyo, wananchi na wakulima kuhakikisha tunapata majawabu ya Matatizo hayo yanayowakabili wananchi.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA KUFANYA KAZI ZA MUDA ZA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 BAADA YA USAILI KUFANYIKA July 27, 2022
  • UPANGISHAJI WA MAJENGO YA OFISI NA NYUMBA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA ZILIZOPO MANISPAA YA SHINYANGA July 02, 2020
  • TANGAZO MAPOKEZI YA FEDHA February 09, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI - Mtendaji wa Kijiji Daraja la III (Nafasi 1) August 13, 2021
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • SHINYANGA DC YAFANYA INTERVIEW ZOEZI LA ANUANI YA MAKAZI NA POSTIKODI

    March 21, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

    March 16, 2022
  • Shinyanga DC yatoa Million mia moja sabini na Tatu na laki nane (173,808,661) kwa makundi ya Vijana, Kina Mama na Watu wenye Ulemavu

    February 03, 2022
  • Shinyanga DC yatoa Million mia moja sabini na moja na laki nane kwa makundi ya Vijana, Kina Mama na Watu wenye Ulemavu

    February 03, 2022
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa